Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwasajili wafanyabiashara wa Chanika, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam ili kuwapatia Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ikiwa ni operesheni maalum iliyoanza jijini ya kuwatambua walipakodi wote. (Picha na Fadhili Akida).
zaidi ya miaka 4 iliyopita
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akigawa miche ya Korosho kwa wanachama wa vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku katika Kata ya Lupa wilayani Chunya ikiwa ni uzinduzi wa kilimo cha zao hilo mkoani Mbeya jana. Zao hilo saa litalimwa katika wilaya za Chunya, Mbarali na Kyela. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa. (Picha na Joachim Nyambo)
Rais John Magufuli akiagana na wanafamilia alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Kangi Lugola aliyefariki jana.
Rais John Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Kangi Lugola aliyefariki jana.
Rais Dkt John Magufuli akisalimiana na Johnson Nguza "Papii Kocha' walipokwenda Ikulu jijini Dar es salaam kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.
Rais John Magufuli akisalimiana na mwanamuziki Nguza Viking "Babu Seya" ambaye pamoja na wanae Johnson Nguza "Papii Kocha', Francis Nguza na Nguza Mbangu walipokwenda Ikulu jijini Dar es salaam kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkesha wakuliombea Taifa Dua maalum wakishangilia kuvuka mwaka 2017 na kuingia mwaka mpya 2018, mkesha uliofanyika katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam chini ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyemwakilisha Rais John Magufuli. (Picha na Brown Kalaita).
Rais Dkt. John Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikabidhi miche ya kisasa ya mikorosho bora kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya million10 iliyofanyika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.