ABIRIA wa daladala ni ‘watiifu’ kweli. Wana ‘nidhamu’ kubwa kwa makondakta. Ukitaka kuthibitisha, wewe ambaye una muda mrefu bila kupanda daladala siku moja jilipue utumie usafiri huu, hususani katika Jiji la Dar es Salaam. Ni kawaida kabisa, abiria wa daladala hata kama amekaa kwenye kiti karibu na dereva, kondakta akiuliza kituo, abiria lazima amgeukie kondakta aliye mlangoni kusisitiza amshushe.