KUBWA linalonikera Kama Mzazi ni lile lililoripotiwa hivi karibuni kutoka wilaya ya Tanga na kwa wale ambao kwa bahati mbaya hawakubahatika kusoma habari hiyo, basi sina budi niwakumbushe kwamba habari hiyo ilihusu biashara ya ngono inayoendeshwa na wasichana wadogo tena waziwazi bila soni wala staha.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
MAMBO vipi mtu wangu, bila shaka upo ‘poa’, na ‘mishemishe si za kitoto’ wakati huu tunapoendelea kupambana na changamoto za kila siku, wape ‘hi’ wadau, tupo pamoja.
JIJI la Dar es Salaam limekumbwa na hofu kutokana na taarifa za kusambaa kwa ugonjwa wa homa ya dengue hasa katika Wilaya ya Kinondoni.
WANASIASA bwana! Walio katika chama tawala, walio kwenye upinzani, wote wanafanana.
SUALA la kuishi nyumbani kwa ndugu na jamaa ni suala lililozoeleka au ni la kawaida katika jamii za Kitanzania, hivyo sio jambo la kushangaza kujikuta ukiishi hivyo.
HIVI karibuni vyombo vya habari vilimnukuu Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Martha Umbula akitoa uamuzi mgumu wa kumnusuru msichana Ngaya Bakari (17) ambaye Februari 4, mwaka huu, baba yake mzazi alimpeleka kwa mume kwa lazima.
SIKU zote mlinzi wa mtoto au watoto ni wazazi au walezi wake, kwani hiyo ndio hali halisi ya wanadamu. Watu hao ndio watu wa karibu zaidi kwake kuliko watu wengine wa pembeni. Hata hivyo hali inaonekana kuwa tofauti kwa baadhi ya wazazi na walezi na wao ndio hugeuka kuwa adui kwa mtoto au watoto wao wenyewe, mpaka unajiuliza ni shetani gani ameingilia ufahamu wa watu wazima ambao walipaswa kuwalinda na kuwatunza watoto.
NAAMINI upo salama, Mungu ni mwema sijambo, siku zinakwenda, maisha yanaendelea. Siku chache kabla ya kuyaandika utakayoyasoma leo niliwasiliana na msichana aliyekuwa anaishi na kufanya kazi jijini Mwanza.
NI kipindi cha neema mkoani Dodoma. Vijijini hali ni shwari. Mashambani kunapendeza. Hakuna mvua bali ni jua lenye neema. Mazao yamekomaa, jua limesaidia kuyakausha tayari kwa mavuno. Siyo tu vijijini ambako neema inaonekana, bali pia mjini. Wanaochoma mahindi ya kuuza wamejaa tele mitaani.
MAENDELEO yanapendwa na kila mtu. Dodoma kwa waliowahi kuja kufanya kazi huku miaka ya nyuma kulikuwa kumezubaa hadi kukawa kunachukiza. Siku hizi acha kusema, kumechangamka sana, licha ya kuwepo Bunge ambao wamelizoea, lakini pia kuwepo taasisi nyingi za elimu nako kumechangia kuichangamsha Dodoma.