HIVI karibuni Shirika la Kazi Duniani (ILO) limewataka waajiri kuwalipa watumishi wa ndani mshahara wa Sh 65,000 kwa mwezi ili kuwatendea haki sawa na waajiri wengine Ili kutekeleza agizo hilo, Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Mahoteli, Majumbani, Huduma ya Jamii na Ushauri (CHODAWU), kinakabiliwa na changamoto ya kuanzisha mfumo utakaowezesha watumishi wa ndani kutambua na kupigania haki zao.