MKOA wa Pwani ni moja ya maeneo, yanayoongoza kwa ajali za barabarani nchini. Sababu mojawapo inayofanya mkoa huo uwe na ajali nyingi ni kupitiwa na barabara kuu. Unapitiwa na barabara kuu iendayo mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Geita, Mwanza na Kagera hadi Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).