KATIKA toleo la leo tumeandika habari kuhusu kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kutoa motisha wa Sh milioni 50 kwa halmashauri 10 zilizofanya vyema na kuwa na hati safi. Kwanza tunapenda kumpongeza waziri mkuu kwa kufikiria kuwapa motisha waliofanya vyema kama njia ya kushawishi utendaji bora zaidi katika halmashauri zetu.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
WAKATI serikali inajitahidi kupeleka nishati ya uhakika vijijini kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA), taarifa tuliyochapisha katika toleo la jana yenye kichwa cha habari 'Wanaopitiwa na REA walalamikia vishoka', haiwezi kupita bila kufanyiwa tathmini.
KATIKA toleo la jana gazeti hili lilichapisha habari yenye kichwa cha habari 'KIU watangaza udhamini kwa wanafunzi 1,800'.
BAADHI ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, wako nchini kwa ajili ya ziara ya kimichezo.
GIZO la Rais Jakaya Kikwete kwa viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro juu ya kuwataka kuacha udhaifu na woga halina budi kuchukuliwa kwa umakini na sio tu kwa Morogoro pekee, bali iwe ni kwa nchi nzima na wale wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao wabanwe.
UTAFITI uliofanywa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), umebaini kuwa vurugu wakati wa uchaguzi ni miongoni mwa sababu za wanawake na watu wenye ulemavu, kushindwa kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi.
JANA katika gazeti hili na leo, pia tumeandika habari kuhusu msimamo wa Tanesco katika ununuzi wa nishati ya umeme kutoka katika mitambo inayofua umeme kwa kutegemea makaa ya mawe, mradi wa NDC na ule wa Wachina wa Ludewa.
HIVI karibuni gazeti hili lilichapisha habari kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha utaratibu wa kufuatilia magari, yanayopeleka mizigo nje ya nchi kwa njia ya kielektroniki.
RAIS Jakaya Kikwete ambaye amebakiza mwaka mmoja tu kustaafu urais, amepata mafanikio makubwa ambayo kila Mtanzania mwenye mapenzi na nchi hii, anajivunia.
MEI mwaka jana, raia watano waliuawa na polisi katika migodi ya North Mara Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara, baada ya watu kati ya 800 na 1,000 wenye silaha mbalimbali za jadi, kuuvamia wakitaka kuchukua mchanga wa dhahabu.
zaidi ya miaka 8 iliyopita