MABASI mengi madogo ya abiria, yafanyayo safari zake kati ya Gongo la Mboto hadi Kivukoni jijini Dar es Salaam, yaliingia katika mgomo juzi, kushinikiza Serikali na mamlaka husika kuwaruhusu kuendelea na utaratibu wao wa zamani wa kufikisha abiria wake hadi mwisho wa basi, yaani Kivukoni.