KAMPUNI ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER), inatarajia kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi mafuta mara mbili zaidi, baada ya kukamilika kwa ukarabati wa matangi yake mawili, yenye mita za ujazo 36,600 kila moja ifikapo Machi mwaka huu.