WIZARA ya Biashara, Viwanda na Masoko imewataka wakulima kuendelea na kasi ya kulima mazao ya viungo ambayo bei yake ni nzuri katika soko la dunia.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
SHIRIKA la Ndege la Taifa (ATCL) mwishoni mwa wiki iliyopita, lilizindua ndege yake mpya aina ya CRJ-100 yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kuongeza idadi ya ndege zake sambamba na kuongeza idadi ya safari zake.
WAFANYABIASHARA na Watanzania wameshauriwa kuzitumia fursa zilizopo mkoani Dodoma, ikiwapo ya kuwa makao makuu ya nchi kuvutia na kuchochea uwekezaji wa ndani na nje ili kusaidia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu.
WATANZANIA wanaotumia huduma za mawasiliano bado wanaendelea kupata huduma hizo kwa gharama nafuu kwa kupiga simu na matumizi ya intaneti ukilinganisha na huduma zinazotozwa kupata mawasiliano katika nchi nyingine za Afrika ikiwemo Afrika Kusini, Kenya, Nigeria na hata nchi ya india.
KAMPUNI ya Simu za mikononi ya Airtel imekabidhi magari manne aina ya Toyota IST kwa washindi wa promosheni ya Airtel Yatosha ambayo inaendeshwa na kampuni hiyo kwa wateja wa bando.
UONGOZI wa Shirika la Masoko Kariakoo, umefanya mawasiliano na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kwa ajili ya kutoa taarifa muhimu za bei za mazao sokoni hapo kila siku.
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limekiruhusu kiwanda cha U-Fresh Food Limited cha Tegeta, Dar es Salaam, kiendelee kuzalisha juisi ya U-Fresh, kwa kuwa kimetimiza masharti ya viwango vya ubora vya juisi hiyo.
BARAZA la Taifa la Biashara (TNBC) limewataka wafanyabiashara mkoani Dodoma kutumia fursa ya wafadhili wa Denmark wenye lengo la kuboresha na kutengeneza mazingira rafiki ya ufanyaji biashara ili wapate manufaa zaidi katika kuendeleza biashara zao.
MKAZI wa Kyela mkoani Mbeya, Edom Mwansasu (40) amekabidhiwa gari aina ya Toyota IST na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel baada ya kuibuka mshindi kupitia droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi, iliyofanyika siku ya Ijumaa iliyopita.
KUTOKANA na Wilaya ya Bunda kutajwa kuwa ni kati ya wilaya masikini nchini, wilaya hiyo imefanya kongamano kubwa la uchumi lililoshirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo ili kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, wilaya na Taifa kwa ujumla.