GAVANA wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu amesema kuporomoka kwa mchango wa sekta ya kilimo katika Pato Halisi la Taifa (GDP) kunatokana na baadhi ya watu vijijini kukacha kilimo; badala yake wamegeukia shughuli zingine za kiuchumi kama sekta ya huduma.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
BALOZI wa Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania amemkabidhi kitita cha Sh milioni moja mshindi wa promosheni hiyo Claudia Mapunda ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika hafla fupi iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
MWANAMKE mchuuzi wa mboga katika Soko jipya la Kawe jijini Dar es Salaam, Grace Pascal Kalengera, jana alikuwa miongoni mwa wakazi watatu wa Dar es Salaam waliokabidhiwa zawadi zao baada ya kushinda promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi.
KAMPUNI za simu za mkononi Tigo na Vodacom zimeungana pamoja katika utoaji wa huduma za fedha kwa njia ya mitandao ambapo kwa sasa wateja wa kampuni hizo watanufaika na huduma za upokeaji na uwekaji wa fedha.
MKAZI wa wilaya ya Magu mkoani Mwanza anayejishughulisha na ujasiriamali James Mangu leo amekabidhiwa kitita cha Sh milioni 10 alizojishindia kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania katika hafla iliyofanyika katika tawi la Benki ya CRDB tawi la Mwanza Mama jijini Mwanza.
WANANCHI wa kata ya Engaruka iliyopo katika Jimbo la Monduli mkoani Arusha wamepongezwa kwa kutoa eneo la ardhi ya hekta 23,000 kwa Serikali ili eneo hilo liweze kutumiwa kujenga kiwanda cha magadisoda.
CHAMA cha Ushirika wa Akiba na Mikopocha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS Saccos Ltd), kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kibenki mwaka huu.
KAMPUNI ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania, Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER), sasa imepanga kuwekeza takribani Sh bilioni 25.6 kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi mafuta kufikia mita za ujazo 300,000.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kuendelea kushuka kwa bei ya mafuta bei ambazo zinaanza kutumika leo.
MKAZI wa Wilaya ya Sengerma ambaye ni mvuvi katika kisiwa cha Yozu, Kijiji Gweso amekabidhiwa gari aina ya Toyota IST jana na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel .