WAFANYABIASHARA wa zao la ndizi Wilaya ya Moshi Vijijini wataanza kunufaika na bei ya zao hilo tofauti na zamani ambapo walikuwa wanalanguliwa na madalali.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetangaza siku 90 kwa wamiliki na wakurugenzi wa makampuni kuwasilisha taarifa zao za mwaka zahesabu za kampuni zao zilizokaguliwa na Mhasibu anayetambuliwa kisheria, vinginevyo kampuni zao zitafutwa na wao kuchukuliwa hatua za kisheria.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imezifungia kampuni 19 kushiriki katika zabuni kwenye taasisi za umma nchini, kutokana na kushindwa kutekeleza kikamilifu mikataba iliyoingia na taasisi za umma na hivyu kusababisha mikataba hiyo kuvunjwa.
KAMPUNI ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) inayomiliki Kampuni ya IPTL imesisitiza kwamba mchakato wa kushusha bei ya umeme kutoka Sh 450 kwa uniti hadi Sh 80 uko mbioni kukamilika.
SERIKALI imefuta msamaha wa kodi kwa kampuni zote za madini nchini, ambapo kuanzia mwakani zitatakiwa kulipa kodi ya mapato yote.
KAMPUNI inayojihusisha na ufuaji umeme nchini ya Aggreko, imezindua rasmi kituo chake maalumu cha uuzaji wa mitambo ya kufua umeme Dar es Salaam, huku ikiitabiria makubwa Tanzania kiuchumi siku za usoni kutokana na uzinduzi wa gesi asilia.
KAMPUNI ya uzalishaji umeme ya PAP/IPTL ipo katika maandalizi ya kushusha bei ya uuzaji umeme kwa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kutoka Sh 450 kwa uniti iliyopo sasa hadi Sh 80 kwa uniti ifikapo mwakani.
SERIKALI imesema kuwa ipo tayari kuwatafutia masoko ya nje wafanyabiashara wa ng’ombe hapa nchini iwapo watajiunga katika vikundi vya ushirika na kufanya biashara kwa kufuata sheria na taratibu.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema taasisi mbalimbali za kimataifa zinazojishughulisha na masuala ya mafuta na gesi zimeanza kujitokeza kuomba fursa ya kuwekeza katika sekta hiyo.