BENKI ya NBC imetangaza washindi wa kwanza wa promosheni ya Weka Upewe, ambayo wateja wenye Akaunti ya Malengo watajishindia pikipiki, bajaji na zawadi kubwa ya gari. Droo hiyo ilichezeshwa katika Tawi la NBC la Mlimani City jijini Dar es Salaam na kusimamiwa na Mkaguzi Mwandamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa, Mrisho Millao.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika kuanzia Novemba 16,mwaka huu kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
VIJANA zaidi ya 1,000 jana walisaini karatasi maalumu yenye ujumbe wa kutaka Serikali kufuta misamaha ya kodi kwa kampuni kubwa.
TAASISI ya kifedha ya Bayport Tanzania, imezindua huduma mpya ijulikanayo kama ‘Mikopo ya Bidhaa’ ikiwa na lengo la kurahisisha utendajikazi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wote wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport.
KAMPUNI ya umma ya uchimbaji mafuta nchini Ufaransa ya Maurel and Prom mwishoni mwa wiki ilikuwa na nafasi ya kuwaelezea waandishi wa Kitanzania walioko ziarani Ufaransa , jinsi wanavyofanya shughuli zao na nini wanatarajia kukifanya nchini Tanzania katika siku za usoni hasa baada ya kuingia mikataba kadhaa ya ushirikiano na kampuni zinazojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa gesi nchini.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Bharti Airtel inayofanya shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika na Asia juzi imetangaza mpango na kuzindua huduma ya kutuma na kupokea pesa Afrika Mashariki.
MSHAURI wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC), Sadruddin Govinji amesema karafuu ya Zanzibar imeendelea kupata umaarufu katika soko la dunia kutokana na sifa zake za kipekee zenye ubora.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali imefungua milango kwa wawekezaji kwenye sekta zote lakini mkazo unaelekezwa zaidi kwenye Sekta ya Afya, Kilimo hasa usindikaji mazao, nishati na miundombinu.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amefanya mikutano na wawekezaji kadhaa ambao wanahudhuria mkutano wa uwekezaji barani Afrika ulioanza jana jijini London, Uingereza. Katika mikutano hiyo, Waziri Mkuu alikutana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited, Baroness Linda Chalker na kujadiliana naye masuala yanayohusu utawala bora.
BENKI ya Akiba Commercial (ACB) imezindua huduma ya ACB Golden Account yenye lengo la kutoa nafasi kwa wateja kujenga tabia ya kujiwekea akiba.