Taifa Stars basi tena CHAN!

NDOTO za timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kufuzu fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN), imepotea baada ya muda mfupi uliopita kufungwa mabao 3-0 na Uganda ‘The Cranes’.

Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa St Mary’s Kitende, mjini Entebbe, nchini Uganda umeifanya Taifa Stars kutolewa kwa jumla ya mabao 4-0, baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Stars kulala bao 0-1.

Mchezo huo wa Dar es Salaam ulisababisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kumuondoa kocha wa timu hiyo,Mdenmark Kim Poulsen na benchi lote la ufundi na kikosi hicho kikawa chini ya kocha wa Namungo FC, Mzambia Honour Janza, akisaidiwa na Mecky Mexime, huku Juma Kaseja akiwa kocha wa makipa.

Habari Zifananazo

Back to top button