Taifa Stars yafuzu Afcon 2023

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ usiku huu imeandika historia nyingine huko nchini Algeria, baada ya kufuzu mashindano ya Afcon 2033, yatakayifanyika nchini Ivory Coast.

‘Stars’ imefuzu kwa kupata pointi 8 katika michezo 6 iliyocheza kundi F, lililokuwa na timu za Algeria waliomaliza na pointi 16, Uganda waliomaliaza na pointi 8 na Niger waliomaliza na pointi 2.

Tanzania imefikisha pointi hizo baada ya kupata sare ya bila kufungana katika mchezo wa raundi ya sita uliopigwa leo nchini Algeria.

Advertisement

Mei 6 2021  Stars iliweka rekodiya kufuzu michuano hiyo baada ya miaka 39.

8 comments

Comments are closed.