Taifa Stars yafuzu tena michuano ya AFCON 2023

ALGERIA, Algiers: Timu ya soka ya wanaume ‘Taifa Stars’ wameibuka mashujaa wa taifa kwa kufuzu Michuano ya Mataifa Afrika kwa mara ya tatu, ‘AFCON 2023’ wakiwa ugenini dhidi ya Algeria, katika dimba la May 19, 1956 nchini Algeria.

Matokeo ya 0-0 ndani ya dakika 90 yameifanya Stars kumaliza nafasi ya pili katika kundi F, kwa alama 8 nyuma ya Algeria vinara wa kundi wenye alama 16 hivyo timu mbili za juu zimekata tiketi ya kushirikia AFCON 2023 itakayovurumishwa huko Ivory Coast.

Ilhali, majirani Uganda ‘The Cranes’ licha ya kupata ushindi wakiwa ugenini 0-2 dhidi ya Niger wamemaliza nafasi ya tatu wakiwa na alama 7 na mkiani yupo Niger kwa alama 2.

Kama ilivyo ada, ‘chanda chema huvikwa pete,’ Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kupitia Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu aliyepo katika msafara wa Stars huko Algeria.

Aidha, Yakubu amewahakikishia Stars kuwa ahadi ya Rais Samia kuwakabidhi Sh Milioni 500 ipo palepale.

“Katika maandalizi ya mechi dhidi ya Uganda kule nyumbani, Mheshimiwa Rais aliahidi kutoa Sh Milioni 500 timu hii ikifuzu. Nafurahi kuwaambia kwamba hizo fedha sio tu kwamba zitatolewa, lakini zimeskwishaletwa wizarani kwaajili yenu,” amesema Kiongozi huyo akiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji.-

Habari Zifananazo

6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button