Taifa Stars yapata kocha mpya

SHIRIKISHO la soka nchini (TFF) limemtangaza Adel Amrouche mwenye asili ya Algeria kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Taarifa iliyotolewa leo Machi 4,2023 na TFF, imeeleza kuwa kocha huyo raia wa Ubelgiji ana uzoefu katika soka kwa kuzifundisha timu kadhaa za taifa katika ukanda wa Kusini, Mashariki, Kati na Kaskazini.

Amrouche amewahi kutwaa tuzo ya kocha bora wa Afrika Mashariki mwaka 2013, baada ya kuipa ubingwa wa Cecafa timu ya Taifa ya Kenya. Aliwahi pia kucheza michezo 20 bila kupoteza.

Kwa nyakati tofauti kocha huyo amewahi kuzifundisha timu za Yemen, Libya, Burundi, Equatorial Guinea, Botswana. Pia aliwahi kuifundisha klabu ya Motema Pembe ya DR Congo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button