Takukuru Mtwara yaokoa Sh milioni 77,000

MTWARA: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mtwara imeokoa zaidi ya Sh milioni 77,000 fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa sekta ya elimu uliyotekelezwa chini ya kiwango wilayani Nanyumbu mkoani humo.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mtwara, Elisante Mashauri amesema ufatiliaji wa utekelezaji wa mradi huo umefanyika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi 2024.

Mradi huo ni ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, matundu matatu ya vyoo na ununuzi wa madawati 45 katika shule ya msingi msinyasi iliyoko wilayani humo.

Advertisement

‘Katika ufatiliaji huo, tulibaini kuwa madawati 45 yote hayakukidhi viwango vya ubora vilivyokubaliwa katika mkataba” ameeleza Mashauri

Hata hivyo milango na vitasa vilivyowekwa havikuwa na ubora kama ilivyoainishwa katika mkataba.

Baada ya kubaini mapungufu hayo walitoa ushauri wa kurekebishwa mapungufu hayo yote na yamefanyiwa kazi hivyo kukidhi viwango vya ubora unaotakiwa.

Pia wamefanikiwa katika ufatiliaji wa miradi mingine 17 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5 yote ikiwa ni ya sekta elimu katika maeneo mbalimbali mkoani humo.