Takukuru yabaini jambo miradi 3 Dar

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ilala, imebaini ukiukwaji wa mikataba, taratibu za manunuzi pamoja na matumizi kutoendana na malengo katika miradi mitatu kati ya sita iliyokaguliwa ikijumuisha sekta za afya, ujenzi, elimu na huduma za jamii.

Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 23, 2023 jijini Dar es Salaam na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilal,a Sosthenes Kibwengo wakati akitoa taarifa ya robo mwaka katika ukaguzi wa miradi sita ya maendeleo mkoani humo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15.

“Kupitia ufuatiliaji huu, miradi mitatu yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni nne, ilionekana na mapungufu ikiwemo ujenzi wa maliwato 30 ya umma Mkoa wa Dar es Salaam unaotekelezwa na DAWASA yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 3, ujenzi wa kituo cha afya Segerea wenye thamani ya Sh milioni 500, sambamba na mradi wa utoaji mikopo ya 10% kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa vikundi 23, ” amesema.

Kibwengo ametaja miradi ambayo utekelezaji wake unaendelea vizuri, ikiwemo ujenzi wa madarasa 255 kwa fedha za UVIKO 19,  mfumo wa ukaguzi wa biashara za hoteli, migahawa na mama lishe, pia ujenzi wa barabara zinazosimamiwa na Kamati ya Ukaguzi ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini TARURA.

Kibwengo amewashukuru na kuwataka wakazi wa Ilala kuendelea kutoa ushirikiano kwa kukataa rushwa, pia wasisite kutoa taarifa popote penye viashiria vya rushwa.

Habari Zifananazo

Back to top button