TANGA; Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Tanga imebaini mapungufu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni tano.
Akiongea na waandishi wa habari Ofisa uchunguzi mwandamizi katika taasisi hiyo Mkoa wa Tanga Frank Mapunda wakati wa kutoa taarifa ya utendajikazi wa taasisi hiyo katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu.
Amesema kuwa mapungufu hayo wameyabaini baada ya kufanya ukaguzi kwenye miradi 60 yenye thamani ya Sh bilioni 10.6 ambapo miradi 28 ndio ilibainika kuwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo ununuzi wa vifaa vilivyochini ya kiwango na ujenzi usiozingatia maelekezo ya ramani.
Aidha katika kutekeleza jukumu la uzuiaji wa Rushwa taasisi hiyo mkoani Tanga imefanikiwa kufanya uchambuzi wa mifumo tisa Ili kupata mifumo imara isiyokwamisha utoaji wa huduma bora Kwa wananchi na utendajikazi za serikali.
Vile vile Mapunda amesema katika utekelezaji wa Programu ya TAKUKURU rafiki wameweza kutembelea kata 22 na kupokea kero zaidi ya 390 za vitendo vya rushwa huku kero 107 zikiweza kupatiwa ufumbuzi.
Comments are closed.