Takukuru yabaini risiti feki za EFD Shinyanga

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru )mkoani Shinyanga imebaini mfumo wa stakabadhi za Mashine za Kielektroniki (EFD) kwa zabuni wanazofanya biashara na halmashauri kuwepo kwa risiti za kughushi.

Ambapo EFD hizi zinautambulisho wa TIN namba ya mfanyabiashara tofauti anayetoa huduma au bidhaa.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy amesema hayo leo Februari 7, 2024  wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kessy amesema “tumeshauri elimu kwa wananchi itolewe  dhidi ya matumizi sahihi ya risiti za EFD na kuanzisha kwa uchunguzi wa risiti za kughushi”.

Amesema katika uchambuzi wa mfumo kuhusiana na utoaji wa huduma za ardhi kupitia mabaraza  ya ardhi ambapo ilibainika wananchi kutokulipa kodi ya pango la ardhi na nyumba baada ya wananchi kufanyiwa umilikishaji.

“Ucheleweshwaji wa kutatua migogoro tumeshauri elimu kwa wananchi itolewe juu ya matakwa ya Sheria yanayopaswa kufuatwa ili wananchi waweze kumiliki ardhi kisheria”.amesema Kessy.

Habari Zifananazo

Back to top button