TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imesema jumla ya malalamiko 58 ya rushwa yameripotiwa katika kipindi cha robo mwaka kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2022.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika ofisi za taasisi hiyo Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi,Fautine Maijo amesema kati ya hayo,taarifa 24 zilikuwa za Serikali za Mitaa, taarifa moja elimu, taarifa nne idara ya ardhi, taarifa moja hifadhi na Polisi taarifa saba.
Aidha, taarifa nyingine ni idara ya fedha na biashasha taarifa moja, idara ya mzingira taarifa moja, idara ya afya taarifa mbili, Maliasili taarifa tatu, ujenzi taarifa mbili, Kilimo taarifa mbili, TFS taarifa nne,Vyombo vya habari taarifa mbili, TASAF tarifa moja, taasisi za dini taarifa moja na binafsi taarifa nne.
Maijo ameongeza kuwa,katika malalamiko hayo sita yalisikilizwa na kutolewa ufumbuzi huku taarifa nyingine zikiendelea kufanyiwa uchunguzi