Takukuru yataka trafiki wabadilishwe vituo

KATAVI; Mpanda. TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Katavi, imependekeza kubadilishwa vituo vya kazi kwa askari wa usalama barabarani, ili kuimarisha uadilifu katika utendaji wa kazi zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi, Faustine Maijo, mapendekezo hayo yanatokana na uchambuzi wa mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kuwa na uadilifu duni.

Maijo amesema imebainika pia kuwepo kwa baadhi ya watendaji wa kitengo hicho kufanya kazi kwa mazoea na kuwepo kwa askari katika eneo moja siku zote, kitendo kinachotengeneza mianya ya rushwa.

Amesema imebainika kuwepo kwa matumizi ya lugha zisizo sahihi kuhalalisha rushwa ikiwemo ‘fedha ya maji au fedha ya kiwi’.

Pia TAKUKURU imependekeza kuchukuliwa hatua stahiki kwa askari wasio waadilifu kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button