TAKWIMU: Wanawake wanaishi zaidi ya wanaume

MTAKWIMU Mkuu wa Serikali, Albina Chuwa amesema kulingana na matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 umri wa kuishi umeongezeka kutoka 65.5 hadi 66.5 ambapo wanawake wanaishi umri mrefu zaidi kuliko wanaume.

Kulingana na matokeo hayo umri wa wanawake kuishi ni miaka 69 huku umri wa mwanaume kuishi ukiwa miaka 62.

Aliyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022 na ugawaji wa magari ya kubebea wagonjwa na vifaa tiba ambapo Rais DK Samia Suluhu Hassan ni mgeni rasmi.

“Mwaka 1978 tulikuwa na watu milioni 17.5 umri wa kuishi ulikuwa miaka 65.

5 na mwaka 2022 umri wa kuishi ni 66.

5 wanawake wakiongoza.

Amesema utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria umefanywa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Marekani.

“Utafiti huu ni wa saba wa kwanza ulifanyika mwaka 1997 na umefanyika na wakala ndani ya serikali ambapo asilimia 99 ya matokeo yamefanyika na Tanzania asilimia moja ni Marekani.

Habari Zifananazo

Back to top button