TAMASHA la kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, linatarajiwa kufanyika Oktoba 14, 2022 ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, likishirikisha bendi mbalimbali za muziki
Akizungumza Dar es Salaam ;leo, Mkurugenzi wa Chocolate Princess Limited, Mboni Masimba, amesema tamasha hilo litajulikana kama Nyerere Day Grand Gala Dance.
“Watu wamezoea kumuenzi Mwalimu Nyerere kupitia siasa, lakini mwaka huu tumeona tumkumbuke kwa tamasha la muziki,” alisema na kuzitaja baadhi ya bendi zitakazotumbuiza kuwa ni Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na Sikinde.