Tamasha la bodaboda, bajaji laja

Tamasha la bodaboda, bajaji laja

TAMASHA la Bodaboda na Bajaji linatarajiwa kufanyika Oktoba 1 mwaka huu, viwanja vya Gwambina, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, muandaaji wa tamasha hilo, Aniceth Pambe (Mc Pambe), amesema tamasha hilo ni mahususi kutambua mchango wa bodaboda na bajaji.

“Bodaboda na bajaji wajitokeze kwa  wingi, litaanza asubuhi hadi jioni, jamii tunatambua mchango wao, wanabeba watu muhimu, lakini hawathaminiwi,” alisema.

Advertisement

Kwa upande wake kiongozi wa madereva bajaji, Tip Lazaro, amewaomba madereva wa bodaboda na bajaji kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kwani kutakuwa na burudani mbalimbali.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *