Tamasha la Injili kufanyika Mwanza

WAIMBAJI wa nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya nchi, wanatarajia kushiriki tamasha la kuombea amani Novemba 6 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa tamasha hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, amesema tamasha hilo litazinduliwa rasmi mkoani Mwanza na litafanyika mikoa mitano.

“Tamasha litapambwa na waimbaji kama Christine Shusho, Rose Mhando na Zabron Singers na waimbaji wengine wengi,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button