Tamasha la muziki kuzinduliwa Agosti 12

TAMASHA la Sanaa ya  muziki jukwaani limepangwa kuzinduliwa rasmi Agosti 12, 2023 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa  jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo ambalo linalotambulishwa kuwa ni ‘Hii ni Afrika’ lina lengo la kurejesha umahiri wa uimbaji wa muziki katika kuigiza.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa taasisi  isiyo ya kiserikali ya Tanzania Bora Initiative(TBI) , Abela Bateyunga ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo amesema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Balozi Dk Pindi Chana.

Amesema pia anatarajia mabalozi kutoka nchi mbalimbali na  viongozi wa sanaa watahuduria onesho hilo.

“Serikali iko tayari kushirikiana katika kurudisha michezo ya kuingiza inayoonesha utamuduni wa Afrika na Tanzania,  wataimba na kuigiza kwa kufanya hivi tutarudisha hadhi ya sanaa majukwani na kuajiri vijana wa kitanzania kutumia vipaji vyao na onesho hilo litakuwa bure,”amesema.

Amesema maonesho hayo yatakuwa endelevu ambapo wanatarajia watu 2000 watahudhuria kwa nyakati tofauti kila wiki.

Aidha, amesema jumla ya washiriki 60 watapanda jukwaa moja ikiwemo wanamuziki wa dansi, maigizo ya jukwaani na wacheza dansi

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Alice Arm
Alice Arm
1 month ago

Looking for Alice Arm seams is the worldwide indigenous nuts for all to nil to everyone.

https://globaljournals.org/GJMBR_Volume15/5-Mining-and-First-Nations.pdf

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x