DAR ES SALAAM: WASANII wa muziki wa injili kutoka mataifa nane wamethibitisha kushiriki kutumbuiza katika tamasha la Pasaka la mwaka huu 2023.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama akizungumza leo Januari 31, 2023 amesema wasanii hao wataungana na wasanii wa ndani na kwamba tamasha la mwaka huu mbali na Dar es Salaam pia litafanyika mikoa yote ya Tanzania bara.
Amesema, maandalizi makubwa kuelekea tamasha hilo yamekwisha fanyika kwa asilimia kubwa na watu wakae mkao wa kula.
“Tamasha la mwaka huu litakuwa ni zuri na lenye shangwe kubwa kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam,”amesema
Tamasha la mwaka huu litafanyika siku ya Jumapili ya Pasaka kauli mbiu ikiwa ni ‘Asante Mungu kwa kutupa Rais Samia Suluhu Hassan, mchapakazi’