Tamasha la teknolojia kuibua wawekezaji
TAMASHA la Teknolojia ya Fedha FinTech limepanga kuibua uwezo wa teknolojia nchini na kuonyesha fursa kwa wawekezaji wa kimataifa Ili kujitosa katika soko la Tanzania na kuimarisha zaidi mfumo wa teknolojia na kuongeza ushirikiano na Tanzania .
Akizungumzia wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo leo Dar es Salaam Mkurugenzi wa Eastern Star Group Deogratius John Kilawe amesema tamasha hilo lina mawazo ya kuibua na teknolojia mpya iliyojaa midahalo na ushirikiano wenye tija, na mitandao isiyo na kikomo ambayo inahusisha akili kubwa zaidi kutoka kwa ulimwengu wa fedha na teknolojia.
Ameongeza kuwa, tamasha la FINTECH lilianza mwaka 2016, ambapo katika tamasha lililopita liliweka maazimio mbalimbali na tathmini ya kutekeleza maazimio hayo na mikakati kwa ajili ya kutekeleza yale ambayo yameshindwa kukamilisha katika kipindi cha nyuma.
Amesema tamasha hilo litatoa fursa kwa wadau wote wa FINTECH kukutana kwa pamoja na kutathmini utekelezaji katika hatua zote ili kuweza kupiga hatua katika kufanikisha hilo.
“Mafanikio ya kuwezesha ujumuishwaji wa sekta ya fedha kuwa rahisi, na kuwa mstari wa mbele wa kukuza Teknolojia ya FINTECH”,amesema.
Aidha, amesema tamasha hilo litawaleta pamoja Afrika Mashariki na kubadilishana ujuzi wa kimataifa kutoka kwa wasomi wakuu, watendaji, na viongozi katika vipindi vilivyofikiriwa upya vinavyohusu kubuni, kujenga na kuhakikisha huduma endelevu za kifedha
Amesema tamasha la FINTECH ndilo tukio kubwa zaidi la Teknolojia ya Kifedha katika Afrika Mashariki, likitoa jukwaa kwa jumuiya ya FinTech kuungana, kushirikiana kwa pamoja.