Tamasha la ZIFF lapata Mkurugenzi mpya

MUONGOZAJI wa filamu nchini Amil Shivji ameushukuru uongozi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Nchu za Jahazi Zanzibar (ZIFF) kwa kumchagua na kumtangaza kuwa mkurugenzi mpya watamasha hilo.

Shivji akipokea kijiti toka kwa mkurugenzi wa awali Profesa Martin Mhando amesema tamasha hilo lenye miaka zaidi ya 26 limemuheshimisha yeye kampuni za filamu nchini pamoja na waigizaji wote nchini.

Awali akizungumza wakati wa kukabidhi nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa zaidi ya miaka 15, Prof. Martin Mhando amemuelezea, Shivji kuwa ni chachu inayohitajika katika uongozi wa Tamasha hilo kutokana na weredi wake katika sanaa.

Shivji ameshatayarisha filamu kadhaa na zimeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa filamu hizo ni pamoja na ‘Vuta N’kuvute’ (2022) na ‘T-Junction’ (2017).

Shivji ni msomi aliyefuzu Chuo Kikuu cha York na mwenye Shahada ya Uzamili ya Sanaa katika Utayarishaji wa Filamu kutoka Toronto, Canada,
lakini pia, ndiye mwanzilishi wa Kijiweni Productions, taasisi ya utayarishaji filamu.

Habari Zifananazo

Back to top button