Tamasha Sauti za Busara kufunguliwa leo Zanzibar

TAMASHA la Sauti za Busara 2024 linatarajiwa kufunguliwa leo usiku visiwani Zanzibar na kuhitimishwa Februari 11 huku zaidi ya wasanii 25 kutoka mataifa mbalimbali wakitarajiwa kupanda jukwaa moja ikiwa ni sehemu ya kuazimisha miaka 21 ya tamasha hilo tangu kuanzishwa kwake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotion Lorenz Herrmann amesema tamasha hilo kama kawaida yake huanza na maandamano ya furaha yanayohusisha wasanii na vikundi mbalimbali kutoka viwanja vya Kisonge hadi Mji Mkiongwe ambapo burudani mbalimbali zitaanza kurindima usiku wa leo.

Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Sholo Mwamba, Wakazi, Tamimu, Mubba, Lwemdo Afrika, Warriors from the east, Africulture, Siti & the band, Brain boy, Mjukuu wa marehemu fela kuti, the brother moves on, Zoe Modiga na wengine wengi.

Lorenz amesema tamasha la sauti za busara la mwaka huu linaongozwa na vijana zaidi lakini halitopoteza maana yake haiba yake ya kitamasha kwa kuwa wanafahamu wanachotakiwa kukifanya.

Amesema kuanzia leo usiku maonyesho zaidi ya 27 yanatarajiwa kuonyeshwa katika majukwaaa matatu kwa siku tatu.

“Sauti za busara imeiweka Zanzibar katika ramani ya matamasha, imeimarisha uchumi wa ndani na kujenga ujuzi pamoja na kukuza maisha ya wazanzibar, Tanzania kupitia sekta ya utalii”, amesema Lorenz

Kauli mbiu ya mwaka huu kwenye tamasha hilo ni ‘Moving Diversity’

“Tamasha hilo litahusisha majadiliano ya wasanii, waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa sanaa na muziki” smesem

Habari Zifananazo

Back to top button