MBUNGE wa Viti Maalumu, Tamima Haji Abass leo amekula kiapo cha uaminifu bungeni.
Aliapishwa asubuhi na Spika wa Bunge, Dk.
Tulia Ackson, wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa nane.
Tamima Abass aliteuliwa kuwa mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM), akichukua nafasi iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Iren Alex Ndyamkama.