Tamisemi yakanusha Dugange kujiuzulu

OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imekanusha taarifa ya kujiuzulu kwa Naibu Waziri wa wizara hiyo anayeshughulikia afya, Festo Dugange ili kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa leo Mei 9, 2023 na wizara hiyo imeeleza kuwa Naibu Waziri huyo anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa kutokana na ajali aliyoipata Aprili 26, 2023.

Aidha, Tamisemi imewataka wananchi kupuuzia taarifa hiyo.

Advertisement