TAMISEMI, COPRA wayajenga

DODOMA: Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Sospeter Mtwale ameongoza kikao kazi kati ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kilichofanyika leo jijini Dodoma katika Ukumbi wa TAMISEMI, kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuanisha maeneo ya ushirikiano kiutendaji.

Akiongoza kikao kazi hicho, Mtwale amesema COPRA ni wadau muhimu wa kushirikiana nao kiutendaji kwani Ofisi ya Rais-TAMISEMI inashughulika na utoaji wa huduma kwa wananchi hivyo kikao kazi hicho kitakuwa na tija katika kuboresha eneo la udhibiti wa nafaka na mazao nchini.

“Kikao kazi hichi ni muhimu sana katika kubadilishana uzoefu na kujadiliana namna bora ya kushirikiana kiutendaji ili wananchi wanufaike na huduma zitolewazo na COPRA na TAMISEMI kwa ujumla,” Mtwale amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) Irene Mlola amesema kikao kazi hicho ni muhimu katika kuimarisha ushiriano wa kiutendaji kati ya COPRA na TAMISEMI.

Aidha, Mlola ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwa na COPRA ambayo ina jukumu kubwa la kuhakikisha taifa linachukua nafasi yake katika kuilisha Dunia.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button