Tamisemi yamsimamisha DED achunguzwe

Wahitimu JKT wapewa kipaumbele ajira

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Nassib Bakari Mmbaga.

Taarifa ya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Msimbira ilieleza kuwa Mmbaga amesimamishwa kuanzia Agosti 30 mwaka huu kupisha uchunguzi.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa Bashungwa aliamua hivyo baada ya Mmbaga kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na utendaji kazi usioridhisha.

Advertisement

Msimbira alieleza kuwa Bashungwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu.