DODOMA: KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeielekeza Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutoa orodha ya shule za sekondari zilizokamilika na ambazo hazijakamilika zinazojengwa kupitia mradi wa kuimairisha ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) awamu ya kwanza.
Agizo hilo limetolewa leo Machi 19, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Denis Londo wakati wa kikao cha kamati hiyo cha kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti fungu 77 kwa mwaka 2023/24 kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Februari 2024 na mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2024/25 kwa mikoa mitatu ya Mara, Dar es Salaam na Njombe.
Kikao hicho kimefanyika katika kumbi za Bunge jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Deogratius Ndejembi, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Sospeter Mtwale pamoja na wakuu wa mikoa yote mitatu.