Tamisemi yatoa maagizo ujenzi wa shule mikoa 26

DAR ES SALAAM; SERIKALI imeelekeza ujenzi wa shule zote za wasichana za mikoa ukamilike ifikapo Desemba mwaka huu ili zianze kutumika Januari mwakani.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), anayeshughulikia Elimu, Dk Charles Msonde, akikariri maagizo ya waziri wa wizara hiyo Mohamed Mchengerwa.

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Rukwa inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP katika eneo la Laela kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, alisema serikali imejipanga kupokea wanafunzi wote wa kidato cha kwanza Januari mwakani, hivyo shule hizo lazima zimalizwe kwa wakati.

Dk Msonde akifafaua zaidi kuhusu ujenzi unaoendelea wa shule mbalimbali alisema kuwa mwaka huu serikali inajenga shule mpya za sekondari 212.

Dk Msonde alilieleza HabariLEO kuwa ujenzi wa shule hizo unatarajiwa kukamilika mwezi huu na unakwenda sambamba na ujenzi huo wa shule 26 za wasichana zinazojengwa kila mkoa Tanzania Bara.

Alisema shule hizo 26 kila moja itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 na awamu ya kwanza ya ujenzi ilianza mwaka jana kwa shule 10 kutengewa bajeti ya Sh bilioni tatu.

Dk Msonde alisema ujenzi na awamu ya pili umetengewa Sh bilioni 1.1 kukamilisha ujenzi wa shule 16 kwenye mikoa 16.

“Serikali imejipanga vizuri, hatuna shaka na hakutakuwa na shida kwa wanafunzi kuhudu madarasa, ifikapo Desemba mwaka huu shule zote hizo zitakuwa zimekamilika tayari kupokea wanafunzi wa Januari mwakani,”alisema.

Dk Msonde alisema pia serikali inaendelea kutekeleza mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP) nchini kwa kujenga shule mpya 1,000 za sekondari katika kila kata isiyo na shule hizo.

Alisema mradi wa SEQUIP inatekelezwa na Tamisemi kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na ulianza kutekelezwa mwaka 2020/21  na utakamilika mwaka  2024/25 kwa gharama ya Sh trilioni 1.

2

“Tulianza na shule 231 na zimekamilika, tukaingia na ujenzi wa shule nyingine 212 za kata  na hivyo tuna shule zilizokamilika 443 na kuna shule nyingine zile za kila mkoa zinajengwa shule ya sekondari ya wasichana ya bweni hivyo tutakuwa na shule zilizokamilika 469 kati ya shule 1,026 zinazojengwa,’’alisema.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button