Tamthilia ya Siri yatabiriwa makubwa

DAR ES SALAAM; KAMPUNI ya Azam Media imetambulisha tamthilia ya kitanzania inazofahamika kama ‘Siri’ ambayo imebeba simulizi na kuleta mapinduzi ya tasnia ya tamthilia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, msimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza amesema kuwa uzalishaji wa tamthia  hiyo umezingatia mahitaji ya soko kwani wametumia vifaa vya uzalishaji wa kisasa na ubora wa hali ya juu,” amesema Mgaza.

Ameongeza kuwa waandaaji wapya wanaongia na kazi zao za sanaa zinazoruka kwenye chaneli hiyo  kuhakikisha wanasimamia ubora wa kazi ili wasije kutoa sababu kwa watu wa pembeni kuwanyooshea vidole na kusema kuwa ilikuwa ni nguvu ya soda tu,” amesema Mgaza.

Pia amesema tamthilia hiyo inachukua nafasi ya tamthilia ya Mchongo itakayofikia tamati Novemba 31, 2023 na Siri kuanza rasmi  Desemba 1 2023.

Kwa upande wake mwongozaji wa tamthilia ya Siri Irene Paul amesema watanzania wakae mkao wa kula kwani tamthilia hiyo ina mengi hususani katika kutunza siri kila mtu anayo siri yake.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button