TAMWA wapongezwa wanawake kuwania uongozi
DAR ES SALAAM; Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kondo Mathew amekipongeza Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa mchango wake mkubwa wa kuhamasisha wanawake nchini kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya TAMWA jijini Dar es Salaam, Mhandisi Mathew amesema mchango huo umewawezesha wanawake wengi nchini kujitokeza kwa wingi na wengine wka sasa ni viongozi wakuthaminiwa kwa taifa hili.
“ Mlitamani kuona wanawake wanakuwepo katika nyanja za uongozi wa kisiasa na sasa tunaona kabisa kwamba serikali yetu inaongozwa na jemedari wetu mkuu wetu wa nchi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan haya ni moja ya mchango mkubwa sana ya kazi mnazoendelea kuzifanya ,“ amesema Mhandisi Kondo.