Tanesco Moro wafafanua ukosefu wa umeme

Watumishi wasioenda likizo wanaiibia serikali

SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO), Mkoa wa Morogoro, limesema kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Msamvu, kimepata hitilafu ndogo ya kiufundi.

Hitilafu hiyo ilisababisha kukosekana umeme kwa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Morogoro, Mvomero na Halimashauri ya Wilaya ya Morogoro.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Fadhili Chilombe, amesema hayo Septemba 15, 2022, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya hitilafu ya umeme iliyojitokeza.

Advertisement

Chilombe amesema hitilafu hiyo ndogo ilitokea Septemba 14, mwaka huu majira ya  saa tano na dakika saba asubuhi, ambapo wataalamu walipambana na kurejesha umeme  saa 5 kwa baadhi ya maeneo kuanza kupata umeme.

Mhandisi Chilombe amesema wataalamu wanaendelea na  matengenezo ya sehemu ya pili na wanatarajia kufanya majaribio mengine, ifikapo saa  nane  mchana wa Septamba 15, 2022,  ili kuangalia upatikanaji wa umeme katika maeneo mengine.

Hivyo amewaomba wananchi mkoani humo kutohusianisha hitilafu ya sasa, ambayo ni ndogo na matukio mengine ya nyuma katika kituo hicho cha kupokea, kupooza na kusambaza  umeme cha Msamvu.