Walezi watajwa mmomonyoko wa maadili

IMEELEZWA wazazi na walezi hawawajibiki katika malezi ya watoto kwenye ngazi za familia hali inayochangia kukithiri kwa vitendo vya mmonyoko wa maadili pamoja na vitendo vya ukatili hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu, Amon Mpanju wakati akifungua mafunzo kwa viongozi wa dini katika Kanda ya Kaskazini kuhusu mwongozo wa malezi ya watoto na familia wa mwaka 2023.

Alisema kuwa hali hiyo imesababishwa na wazazi na walezi kutumika muda mwingi katika shughuli za utafutaji wa kipato Kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa familia na kusahau jukumu la malezi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon
Mpanju alisema kuwa lengo la serikali kuja na mwongozo wa malezi ni Kwa ajili ya kuja na mbinu bora za malezi ambazo zitaweza kumsaidia mtoto wa kitanzania kukuwa katika misingi inayozingatia uchamungu na maadili ya kitanzania.

“Tumekutana hapa na viongozi wa dini tunajua nyie ndio msingi wa jamii Bora hivyo kupitia nyie mtatusaidia kuja na mawazo bora ambayo yatamaliza changamoto ya mmonyoko wa maadili katika jamii yetu”alisema Niabu Katibu huyo.

Nao baadhi ya viongozi wa Dini waliipongeza serikali kwa kuja na muongozo huo ambao umehisisha maoni ya viongozi wa dini hivyo utasaidia kuleta matokeo ya haraka.

“Tunajua sisi viongozi wa dini ndio tunajukumu kubwa la kujenga Imani na tabia njema kwa jamii yetu hivyo Kupitia mwingi huu tutaweza kuja na suluhisho la changamoto ambazo zinaikabili jamii hususani vitendo vya Ukatili wa kijinsia. “alisema Shehk wa Mkoa wa Tanga Juma Luuchu.

Habari Zifananazo

Back to top button