Tanga kuzalisha Tani 80,000 za Mkonge ifikapo 2025

TANNGA: Mkoa wa Tanga umejipanga kuzalisha tani 80,000 za zao la mkonge ifikapo mwaka 2025 Ili kuchangia lengo la serikali ya kuzalisha tani 120,000 mwaka 2025/26.

Hayo yamesemwa na Mkurungenzi Mkuu wa bodi ya mkonge nchini Saad Kambona wakati akiongea na wakulima wadogo wa Chama Cha ushirika (Amcos) ya Magoma.

Amesema kuwa uzalishaji Mkonge nchini kwa asilimia kubwa unategemea Mkoa wa Tanga hasa Wilaya ya Korogwe ambapo kwa kipindi cha mwaka 2022/23 uzalishaji Mkonge ulikuwa tani 48,000 nchini.

” Mkoa wa Tanga pekee ukichangia tani 33,000, huku Wilaya ya Korogwe ikitoa tani 14,000 na katika tani hizo 14,000 wakulima wadogo wamechangia tani 7,000.

“Amesema Kambona.

Nae Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga, John Henjewele ameiomba Bodi kuwapatia Amcos maeneo ya mashamba Ili kuongeza uzalishaji na hivyo kuinua vipato vya wanachama na Vyama vya ushirika.

Meneja wa Amcos ya Magoma, Maneno Jackson ameiomba serikali kuweka jtihada kubwa kwa wakulima wadogo Ili waweze kuongeza uzalishaji kutokana na jitihada zao ambazo wameweza kuzionyesha katika msimu uliopitia.

Habari Zifananazo

Back to top button