Tanga wamuenzi Nyerere kwa usafi Mwanzange

OFISI ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, imeshiriki kumbukumbu ya miaka 23 ya kifo cha Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa kufanya usafi wa mazingira kituo cha wazee Mwanzange.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa, amewataka vijana kuwa wazalendo kwa nchi yao, ikiwa ni sehemu ya kulinda tunu iliyoachwa na Baba wa Taifa.

“Tujihadhari na chokochoko ambazo zina mlengo wa kuleta fujo na kuharibu amani ya nchi yetu, ni jukumu letu kuhakikisha tunalinda tunu za nchi yetu, kama ambavyo tulivyoachiwa na waasisi wa Taifa hili,”alisema Mgandilwa.

Habari Zifananazo

Back to top button