Tanga yajipanga kilimo cha mwani

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu jiji la Tanga limejipanga kuwa kinara katika uzalishaji wa majongo bahari, unenepeshaji wa kaa pamoja na kilimo cha mwani kwa kutumia fursa ya bahari iliyopo kwenye Ukanda wa Pwani.

Ummy amesema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya Uchumi wa Bluu pamoja na ya kupendezesha Jiji hilo inayofadhiliwa na Botner foundation.

Amesema kuwa kupitia fursa ya uchumi wa bluu wananchi wataweza kujiongezea fursa ya shughuli za kiuchumi lakini na kujiongezea kipato kupitia fursa za ufugaji na kilimo kupitia bahari.

“Tanga tunaeneo kubwa la bahari tayari mafanikio tumekwisha kuyaona hivyo tumejipanga kuongeza uzalishaji Ili tuweze kuwa vinara wa kutumia fursa za uchumi wa buluu Kwa maendeleo ya watu wetu sambamba na nchi kupata mapato yake”amesema Waziri Ummy.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button