Tanga yajipanga uzalishaji mwani

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema jiji la Tanga limejipanga kuwa kinara katika uzalishaji wa majongo bahari, unenepeshaji wa kaa pamoja na kilimo cha mwani hapa nchi kwa kutumia fursa ya bahari iliyopo kwenye Ukanda wa Pwani.
Ummy amesema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya Uchumi wa Bluu pamoja na ya kupendezesha Jiji hilo inayofadhiliwa na Botner foundation.
Amesema kupitia fursa ya Uchumi wa Bluu wananchi wataweza kujiongezea fursa ya shughuli za kiuchumi lakini na kujiongezea kipato kupitia fursa za ufugaji na kilimo kupitia bahari.
“Tanga tunaeneo kubwa la bahari tayari mafanikio tumekwisha kuyaona hivyo tumejipanga kuongeza uzalishaji Ili tuweze kuwa vinara wa kutumia fursa za uchumi wa buluu Kwa maendeleo ya watu wetu sambamba na nchi kupata mapato yake.”amesema Waziri Ummy.
Mwakilishi mkazi wa shirika la Botner foundation Dk Hassan Mshindo amesema kuwa wawekezaji zaidi ya sh Bil 7.5 katika sekta ya uchumi wa bahari pamoja na kupendezesha madhara ya Jiji la Tanga.
“Fedha hizo Kwa sehemu kubwa zimepelekwa Kwa vijana Ili waweze kujipatia ajira lakini na kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira iliyopo.”amesema Dk Mshindo.