Tanganyika yasaini mkataba mpya biashara hewa ukaa

KATAVI: Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi imesaini mkataba mpya wa biashara ya hewa ukaa baina yao na Taasisi ya Carbon Tanzania huku suala la uaminifu likisisitizwa baina ya pande zote mbili.

Mkurugenzi wa miradi, David Beroff kutoka Taasisi ya Carbon Tanzania wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba huo,amesema kuwa katika mkataba wa awali waliiamini halmashauri hiyo na haikuwaangusha.

“Mtu ambaye anawekeza inamaanisha tayari anakuamini kwa sababu kama huamini huwezi kuwekeza,tunawaamini kutoka mwanzoni na tunawashukuru hamjatuangusha” amesema Beroff.

Advertisement

Nae Mratibu wa biashara ya Kaboni kutoka Tamisemi, Hawa Mwechaga amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia makubaliano ya kimataifa ya kushirikiana na dunia kupunguza ongezeko la  joto nchini ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika inatajwa kama mfano kutokana na kufanikiwa katika biashara ya kaboni.

Amezitaka halmashauri nyingine nchini kuiga mfano huo ili kutimiza adhma iliyokusudiwa na Serikali.