Tangazeni zabuni za skimu za umwagiliaji mapema

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameiagiza Serikali kutangaza haraka zabuni za miradi ya skimu za umwagiliaji Ili utekelezaji wake uanze mara moja.

Chongolo ametoa agizo hilo jana katika mkutano uliokutanisha wananchi katika Wilaya ya Bahi ambapo Katibu wa shina hilo, Joseph Chipule alipomueleza kuhusu changamoto ya ubovu wa miundombinu ya skimu za umwagiliaji.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Bahi, Keneth Nollo alisema wananchi wa eneo hilo wanaojishughulisha na kilimo cha mpunga, wanauwezo wa kulisha Mkoa wa Dodoma endapo skimu za umwagiliaji zingekarabatiwa.

Kaimu Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Dodoma kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mary Mboya amesema Wilaya ya Bahi ina skimu 16 za umwagiliaji huku baadhi zimepangwa kutekeleza mwaka wa fedha 2023/24.

Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Sh bilioni 375 katika mwaka 2023/2024 kwa lengo la kuongeza eneo la umwagiliaji lenye jumla ya hekta 256,185.46 kwa kukamilisha ujenzi wa skimu, kukarabati skimu zilizochakaa, kujenga skimu mpya na mabwawa ya kuvunia maji ya umwagiliaji.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kim
Kim
3 months ago

Make money online from home extra cash more than $18000 to $21000. Start getting paid every month Thousands Dollars online. I have received $26000 in this month by just working online from home in my part time. every person easily do this job by.

Just Open This Website………>>> http://www.Richcash1.com

Last edited 3 months ago by Kim
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x