Tani 2 madini ya uranium asilia zapotea Libya

Tani 2 madini ya uranium asilia zapotea Libya

JUHUDI zinaendelea kutafuta zaidi ya tani 2 za madini ya uranium asilia yaliyoripotiwa kupotea kwenye hazina ya madini hayo huko nchini Libya, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limesema.

Msemaji wa shirika hilo aliiambia CNN kwa barua pepe kuwa: “Takriban tani 2.5 za madini ya uranium asilia, hayakupatikana wakati wa ukaguzi uliofanyika Machi 14.

“Wakaguzi wa shirika la IAEA waligundua kuwa magunia 10 yaliyokuwa na takriban tani 2.5 za madini ya uranium asilia katika mfumo wa mkusanyiko wa madini ya uranium hayakuwepo kwenye eneo lililotangazwa awali katika Jimbo la Libya.”

Advertisement

“Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi amewaalika wajumbe wa shirika hilo na maofisa wanaofanya kazi ili kubaini kilichotokea kwa uranium hiyo na ilipo sasa, “ iliongeza taarifa hiyo.

Katika taarifa siku ya Alhamisi, IAEA ilisema kuwa upotevu wa madini hayo ya uranium “haukuleta hatari yoyote ya mionzi lakini inahitaji kushughulikiwa kwa usalama.”

“Kupotea kwa maarifa juu ya mahali pa sasa pa nyenzo za nyuklia kunaweza kuwa na hatari ya mionzi pamoja na wasiwasi wa usalama wa nyuklia,” ilisema taarifa hiyo, bila kufichua haswa eneo lililopotea madini hayo nchini Libya.

/* */