WAKALA wa Huduma za Barabara (Tanroads) imetangaza kuja na mpango wa upanuzi wa mtandao wa barabara kuu mjini Geita kwa mfumo wa njia nne umbali wa Km 24 ili kupunguza msongamano.
Upanuzi huo wa barabara unaenda sambamba na ujenzi wa njia mchepuko (By pass) ili kupunguza adha ya magari makubwa kupita katikati ya mji wa Geita iwapo hakuna ulazima.
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Geita, Daniel Magogo ametambulisha mpango huo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geita na kueleza lengo ni kuufungua mji wa Geita.
Ameeleza mradi wa upanuzi wa barabara kwa njia nne kwa sasa upo kwenye hatua ya upembuzi yakinifu na mara baaada ya kukamilika tenda itatangazwa na gharama ya mradi itafahamika.
“Mji wa Geita unakua kwa kasi sana, kwani kwa uchimbaji na biashara ya dhahabu, Geita ndio inaongoza, kwa hiyo mji wetu unakabiliwa na ongezeko kubwa la magari,” Amesema.
Amesema mpaka sasa mkoa wa Geita una mtandao wa barabara wa Km 1019.
13 katika mtandao huo kuna km 236 ambazo ni barabara kuu na zilizobaki ni barabara za mkoa.
“Katika mtandao wote wa barabara tuna kilomita 401 ambazo ni barabara za lami kwa mkoa mzima hapo inajumuisha madaraja na makalavati 305.