Tantrade kujikita kwenye masoko ya nje

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imedhamiria kukuza na kuimarisha biashara ndani na nje ya nchi pamoja na kuendeleza chapa ‘branding’ kwa kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

Mkurugenzi wa Tantrade, Latifa Mohamed Hamis amesema mamlaka hiyo inakabiriwa na changamoto ya utapeli ambao unafanywa na wananchi wasio wazalendo pamoja na uchakavu wa miundombinu katika viwanja vya sabasaba.

Amesema mamlaka hiyo imefanikiwa katika masoko ya nafaka, bidhaa za vyakula ,mbao, mashudu, asali na viungo.

Amesema Trantrade inatekeleza majukumu kwa weledi Ili kifikia lengo la serikali kuwa kitovu cha biashara na masoko katika nafaka, bidhaa za vyakula, asali, mbao na viungo kwa kuendelea kukuza na kutangaza bidhaa na huduma ndani na nje ya nchi.

Akizungumza kwa niaba  ya wahariri, Neville Meena  ameshauri mamlaka kutoa taarifa maalum ambayo itasaidia jamii Ili kupunguza taarifa zisizo sahihi katika mitandao ya kijamii.

Hayo yakiwa ni maelekezo ya msajili wa hazina taasisi za umma na sekta binafsi kuongea na wahariri na vyombo vya habari juu ya majuku wanayotekeleza pamoja na malengo yao.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button